Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Bomet District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Bomet District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007

JINA:…………………...........................………………………………….. NAMBARI: ....…………
SHULE: …………….......................…………………………………………………………………….
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI/AGOSTI 2007
MUDA: SAA 2 ½
JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA
BOMET 2007
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA
(K.C.S.E)
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO
 Jibu maswali yote.
 Majibu yako yaandikwe kwenye nafasi zilizoachwa katika kijitabu cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa kumi zilizopigwa chapa. Mtahiniwa ahakikishe kwamba kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma tarifa hii kisha ujibu maswali.
Asifuye mvua imemnyea. Huu ni msemo wenye hakika isiopingika, na kutilia shaka ni sawa na
kudai jua linaweza kubadilika na kuchomozea upande magharibi badala ya mashariki.Huu ndio ukweli uliodhihirika juzi katika vyombo vyetu vya magazeti.
Lisemwalo lipo, na kama halipo li njiani.Waama, pafukapo moshi pana moto. Mwanafunzi mmoja
wa kike kwa jina P.N. katika chuo kikuu kimojawapo nchini alishangaza umma wa Kenya na
ulimwengu kwa jumla alipodai kuwaambukiza wanafunzi wenzake wa kiume mia moja na ishirini na wanne virusi vya ukimwi.
Kisa na maana? Aliambukizwa ukimwi na mwanafunzi mwenzake aliyekuwa akifanya majaribio
ya ualimu katika shule yao ya upili. Baada ya kushawishika sana alijuana naye kimwili, na matokeo yakawa kifo ambacho sasa alikuwa anawagawia wenzake.
Kisa kama hiki kinachangia kueleza kina kirefu cha kutamauka na upweke ambao maisha ya waja
wengi yameingia kiasi cha kuwaacha wanyama ijapo wanaenda kwa miguu miwili bado. Katika
mojawapo ya mafunzo ya kidini ambayo padre alinifunza mimi na wanafunzi wenzangu, tuliambiwa kisasi ni chake Mola, sisi waja wetu ni kushukuru tu. .Mbona basi mwanafunzi kama huyu kutaka kulipiza?
Ima fa ima, na waswahili husema, “mlaumu nunda na kuku pia”.Huyu mwanafunzi hawezi
kuachiwa atende alivyotenda. Aliyekula naye raha alikuwa mtu aliyefahamika vizuri sana kwake.
Isitoshe, huenda wakati huo alikosana na mama na baba kulala nje. Huenda alikosana na ndugu zake kwa kuepa nyumbani usiku wa manane kwenda kumwona huyu kalameni. Huenda alikosana na mwalimu wake kwa sababu kiburi kilianza kuingia. Kwa vyovyote vile, alikula raha na hastahili kuwaadhibu watu wasio na hatia kufidia makosa yake. Je, kama yeye na huyo jamaa wasingekuwa na ukimwi, raha kiasi gani wangezila hadi leo?
Jamii na watu wote kwa jumla hawana budi basi kulaani vitendo vya P.N. vya kuambukiza
wanafunzi wenzake virusi huku akijua. Hili kosa ambalo linastahili adhabu ya kifo. Dawa ya moto ni moto ni adhabu inastahili kuchukuliwa haraka ili P.N. ambaye tayari amekiri hatia, atiwe nguvuni na adhabu itolewe.
Barua ya PN inafafanua jambo jingine sugu. Kwamba kiwango cha maadili katika vyuo vyetu
kimezorota kiasi cha kufanyiana unyama usiosemeka.Vijana wengi siku hizi wanashiriki tendo la ndoa bila haya. Huu upotofu wa maadili katika jamii wapaswa kushutumiwa na wote. P..N. hana sababu yoyote ya kibinadamu, kidini au kitu chochote kile kudai haki kwa uovu huo wake.
Maswali
1. Taja kichwa mwafaka kwa makala haya. (alama 2)
........................................................................................................................................................
2. Katika aya mbili za kwanza, mwandishi anamlaumu mwanafunzi kwa kosa gani? (alama 2)
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
3. Eleza chanzo cha tabia za P.N. (alama 2)

4. Mwandishi wa taarifa hii anataka P.N. achukuliwe hatua gani? Kwa nini? (alama 4)
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
5. Barua ya P.N. bila shaka imeonyesha uvumbuzi mpya. Utaje (alama 2)
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
6. Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika taarifa: (alama 3)
(a) Kina kirefu cha kutamauka
……………………………………………………………………………………………
(b) Ima fa ima
……………………………………………………………………………………………
(c) Kufudia makosa yake
………………………………………………………………………………………...
2. UFUPISHO (ALAMA 15)
Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya mioyo yetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu.Tukumbuke,”Ajizi ni nyumba ya njaa ”. Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga.
Lazima tufanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja.Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima, kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu.Tunahitaji taifa lenye watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbali mbali ya maendeleo.Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao mashambani, kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeke. Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya hayo pia lazima tujishugulishe na biashara ambapo kwa sasa ni wakenya wachache sasa ambao wanatambua umuhimu wa biashara.
Wengi ni wale wenye mawazo ya kwamba lazima kila mmoja aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wengine ambao hawahusiki.
Mafunzo tunayopata majumbani, shuleni, na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua
mbinu ya kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya mwanakenya kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao inayotupumbaza na kutufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa siku zijazo tuwe kielelezo chema kwa wengine. Watu lazima washirikiane na kufikiria kwamba wao ni wamoja,”Utengano ni uvundo”. Lugha ya taifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuweza kutuwasilishia mapendekezo, mawaidha na hisia zetu. Kukosa ndiko kibinadamu ,wakati tunapokosea, lazima tukubali tumekosa na kufanya masahihisho mara moja kwani, “Usipoziba ufa utajenga ukuta”.Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu na wenzetu. Lazima tujitoe mhanga na kupigania nchi yetu tukiwa wazalendo halisi.
Sisi tukiwa vijana sharti tujishugulishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia ya kutatua matatizo hayo siku zote tutekeleze nidhamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashutumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuleni na majumbani mwetu.Utamaduni wa asili unakariri sana kuwa na nidhamu shuleni na majumbani mwetu. Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeleo, amani na upendo, lazima tuwe na bidii, ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo.Tukiwa viongozi ambao hawajishugulishi na maendeleo,basi tutabaki nyuma kama mkia siku zote. Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama kama kwa utajiri wake.Kwa hivyo, basi tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na nasaba kubwa au tajiri.
(a) Eleza dhamira ya mwandishi kwa taarifa hii (maneno 20) (alama 2)
NAKALACHAFU
..............................................................................................................................................................

NAKALA SAFI

……………………………………………………………………………………………………….
(b) Kwa mujibu wa aya ya kwanza, mwandishi awahimiza vijana kufanya nini ili kuleta maendeleo
nchini? (maneno 70) (alama 4)
NAKALA CHAFU
..............................................................................................................................................................
..............................................................................................................................................................
...........................................................................................NAKALA SAFI
..............................................................................................................................................................
..............................................................................................................................................................
..............................................................................................................................................................
..............................................................................................................................................................
..............................................................................................................................................................
...........................................................................................(c) Kulingana na taarifa hii ni mambo gani hasa ambayo yamechangia maendeleo kuzorota nchini
Kenya? (maneno 40 - 50) (alama 6)

SEHEMU B
3. MATUMIZI YA LUGHA: ( ALAMA 40)
(a) Ziandike sentensi zifuatazo ukitumia kiwakilishi cha pekee o-ote. (alama 2)
(i) Ufunguo wowote ufunguao ni wetu.
……………………………………………………………………………………………
(ii) Ngozi zozote zirarukazo ni za kifaru.
……………………………………………………………………………………………
(b) Taja sauti zozote nne zinazotamkiwa katika ufizi. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(c) Andika sentensi inayoonyesha ‘ki’ ya masharti. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
(d) Onyesha viambishi awali na tamati katika kitenzi: Alimkemea. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………
(e) Bainisha matumizi ya ‘ni’ katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
(i) Ondokeni.
……………………………………………………………………………………………
(ii) Kiptoo ni mwizi sugu
……………………………………………………………………………………………
(f) Eleza maana nne zinazojitokeza katika sentensi hii. (alama 2)
(i) Alimpigia simu
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(g) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia matawi. (alama 3)
(i) Vile vingali vikitengenezwa
(h) Akifisha sentensi ifuatayo. (alama 3)
(i) puka chaka hata wewe siamini.
……………………………………………………………………………………………
(i) Eleza tofauti kati ya sentensi hizi mbili. (alama 2)
(i) Ungesoma kwa bidii ungepasi mtihani.
(ii) Ungalisoma kwa bidii ungalipasi mtihani.
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(j) Andika sentensi moja kwa kutumia ‘licha ya’. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(k) Andika ukubwa na udogo wa neno rununu. (alama 1)
(i) Ukubwa ……………………………………………………………………………
(ii) Udogo ……………………………………………………………………………
(l) Andika sentensi zifuatazo kwa wingi. (alama 3)
(i) Domo limepinduliwa.
……………………………………………………………………………………………
(ii) Kiwiko kimejigonga ukutani.
……………………………………………………………………………………………
(iii)Ukimwi umeangamiza wengi duniani.
……………………………………………………………………………………………
(m) Unda vivumishi kutokana na maneno yafuatayo. (alama 2)
(i) Imani
……………………………………………………………………………………………
(ii) Ubora
……………………………………………………………………………………………
(n) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendesha. (alama 2)
(i) – nya ……………………………………………………………………………
(ii) - cha ……………………………………………………………………………
(o) Taja maana mbili ya neno ‘mjomba’. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(p) Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa. (alama 2)
“Ala! Huna heshima wewe mtoto!”
Mama alimkaripia bintiye
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(q) Kamilisha methali zifuatazo. (alama 2)
(i) Ukuni juu ya uchaga ...................................................................
(ii) Simbiko haisimbuki ila ...............................................................
(r) Eleza maana ya misemo ifuatayo. (alama 3)
(i) Msumari wa moto juu ya kidonda.
……………………………………………………………………………………………
(ii) Pasulia mbarika.
……………………………………………………………………………………………
(iii)Giza la ukata.
……………………………………………………………………………………………
10
(s) Onyesha kirai nomino, kirai kivumishi na kirai kielezi katika sentensi. (alama 3)
(i) Bawabu mzuri huandika ripoti ndefu mara kwa mara.
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
SEHEMU C
ISIMUJAMII (ALAMA 10)
Soma nakala hii kasha jibu maswali
“Ni ya leo mama ni ya leo.Ni ya leo baba ni ya leo. Bidii yako ndiyo bahati yako.Tishati na
hamsa, shati arubaini........Mali kutoka ng’ambo; chagua ufungiwe. Ni ya leo, ni ya
leo..............”
MASWALI
(a) Taja mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika makala haya. (alama 4)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(b) Huku ukirejelea makala, pambanua watumizi na mahali pa matumizi. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(c) Taja sifa za lugha inayopatikana katika sajili hii. (alama 4)
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………

More Question Papers

Popular Exams

Return to Question Papers