Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Trans-Nzoia District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Trans-Nzoia District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/3
KISWAHILI
1. HADITHI FUPI
MAYAI WAZIRI WA MARADHI: E KEZILAHABI
a) Eleza maudhui yafuatayo yanavyojitokeza katika hadithi ya mayai waziri wa maradhi
(al 12) *TRZ*
i) Ukombozi
ii) Uongozi mbaya
b) Toa na ueleze mifano yoyote minne ya jazanda zilizotumiwa katika hadithi hii ya
mayai waziri wa maradhi (al 8) *TRZ*
2. TAMTHILIA
KIFO KISIMANI:KITHAKA WA MBERIA
Anwani ya kifo kisimani inaoana vyema na yale yaliyomo katika tamthilia. Jadili kauli
hii kwa kutoa mifano (al 20) *TRZ*
3. Thibitisha vile wanawake wanachukua nafasi kubwa katika ukombozi wa wanabutangi
4. RIWAYA
MWISHO WA KOSA
Jadili matumizi ya mbinu hizi kwa kutoa mifano maridhawa
i) Kinaya (al 12) *TRZ*
ii) Vijembe (al 8) *TRZ*
5. Samahani, Bwana Selele, lakini nimekuja kwa dharura kubwa ya muhimu, hivi
nimeacha teksi hapo nje inanisubiri’’
a) Ni mhusika gani anasema haya (al 2) *TRZ*
b) Kwa nini anasema kuwa amekuja kwa dharura kubwa. Eleza kwa kina
(al 10) *TRZ*
c) Taja sifa zozote nne za mhusika huyu (al 4) *TRZ*
d) Onyesha umuhimu wa Bw. Selele katika riwaya ya mwisho wa kosa
(al 4) *TRZ*
6. i) Una moyo gani N’nakuuliza Wangu mhisani
Na kiasi gani Unavyojiweza Ijapo tufani
Ukiwa laini Utajipoteza Usijibani
Kusimama Pweke Kwataka Makini
ii) Zitavuma pepo Zitapupuliza Uanguke chini
Ela uwe papo Unajikweleza Na kujiamini
Utikiishapo Umejiuiza Pigo la moyoni
Kusimama Pweke Kwataka Makini
iii) Utie migati Ya kutuoteza Hapo aridhini
Kwa nia na dhati Usiogeuza Au kuihini
Zidate baruti Uwe wapuuza Welele usoni
Kusimama Pweke Kwataka Makini
iv) Sishike vishindo Na mauzauza Ya kukuzaini
Kita kama nyundo Ukinuiliza Unayoamini
Na uje mkondo Utadikimiza Kujipa mizani
Kusimama Pweke Kwataka Makini
v) Wengine wasiwe Unaoweleza Yaliyo maani
Wewe ndiwe Unaoweleza Yaliyo maani
Ela kichukuwe Pia kujikaza Katika midani
Kusimama Pweke Kwataka Makini
a) Lipe kichwa shairi hili (al 2) *TRZ*
b) Kwa nini kusimama pweke “kwataka makini ’’ (al 2) *TRZ*
c) Ni hatua gani zinazopendekezwa mtu anayenuia kusimama pweke? (al 5) *TRZ*
d) Andika arudhi za shairi hili (al 5) *TRZ*
e) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi hili (al 6) *TRZ*
i) Muhisani
ii) Migati
iii) Vishindo
iv) Kweleza
v) Mizani
7. Fasihi simulizi
a) Eleza maana ya tanzu zifuatazo za fasihi simulizi (al 8) *TRZ*
i) Miviga
ii) Mighani
iii) Visasili
iv) Ngano
b) Taja sifa nne za mtambaji katika fasihi simulizi (al 4) *TRZ*
c) i) Eleza maana ya ngomezi (al 2) *TRZ*
ii) Toa sifa za ngomezi (al 6) *TRZ*






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers