Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Keiyo District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Keiyo District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



102/3
KARATASI 3
1 USHAIRI
soma shairi hili kisha ujibu maswali.
Jukwani naingia, huku hapa pasokota,
Kwa uchungu ninalia,hii tumbo nitaikata,
Msiba mejiletea,nimekila kiso takata,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?
Wazee hata vijana,wote umewasubua,
Huruma nao hauna,heshima kawakosea,
Ukambani na Sagana,hata mbwa wararua,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?
Wahasibu ofisini,kibwebwe mejifunga,
Miaka mingi vitabuni,ili wasikose unga,
Nadhari wanadhamini,hesabu wanazirenga,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?
Wapenzi wa kiholela,pia wanakuogopa,
Baada yao kulala, wana wao wanatupa,
Wakihitaji chakula,wanachokora mapipa,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?
Wafugaji hata nao,kama dawa wakwamini,
Hawajali jiranio,wamesusia amani,
Wanaiba ng'ombe wao,na kuzua kisirani,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?
Nayo mizozo ya maji, kaonekana kwa mara,
Hiyo nayo ni dibaji,sababu sio harara,
Njaa wahepe wenyeji, huo ndio mkarara,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?
Ningeweza kukuuza,ingekuwa siku njema,
Tena kwa bei ya meza,sokoni nimesimama,
Wala tena singewaza,kuhusu wali na sima,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?
Hatima umefikika,naenda zangu nikale,
Mate yanidondoka,kwa mnukio wa wale,
Naomba kwenda kukaa,wala sio nikalale,
We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?
Maswali
i Lipe anwani mwafaka shairi hili. (Alama 2) *Kyo*
ii Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 2) *Kyo*
iii Huku ukitolea mifano mwafaka, taja arudhi zilizotumiwa katika ubeti wa tatu. (Alama 4) *Kyo*
iv Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (Alama 4) *Kyo*
v Thibitisha kuwepo kwa idhini ya ushairi. (Alama 2) *Kyo*
vi Taja madhila anayoelezea mtunzi wa shairi hili yaletwayo na tumbo. (Alama 4) *Kyo*
vii Elezea maana ya maneno yafuatayo. (Alama 2) *Kyo*
(a) Dibaji
(b) Harara
TAMTHILIA: KIFO KISIMANI,KITHAKA WA MBERIA
2 (a) Elezea sifa zozote tano zinazo mwezesha Mwelusi kupigania haki za watu katika nchi ya Butangi
(Alama10)
(b) Elezea umuhimu wa wahusika wafuatao. (Alama10)*Kyo*
i Bokono
ii Kaloo
iii Askari I
iv Gege
v Batu
3. Onyesha jinsi Kithaka wa Mberia alivyofaulu kupitisha ujumbe wake akitumia mbinu hizi
(Alama20)*Kyo*
i Sadfa
ii Mhusika ndani ya mhusika
iii Jazanda
iv Taharuki
v Ndoto
R1WAYA: MWISHO WA KOSA.Z.BURHANI.
4. "Rashid,nimekwambia zamani kuwa mimi huru, hiari yangu wapi ninakaa au kwa nani,si kazi yako."
a) Elezea muktadha wa maneno haya (Alama 4) *Kyo*
b) Ni uhuru wa aina gani anaolilia mzungumzaji. (Alama 2) *Kyo*
c) Elezea tabia za mhusika aliyetoa maneno haya kwa mujibu wa dondoo hili. (Alama 4) *Kyo*
d) "Uhuru unapokosa kuwa na mipaka huweza kumpotosha mtu." Elezea jinsi ambavyo wazo hili
lilidhihirishwa na mzungumzaji ukirejelea Riwaya ya Mwisho Wa Kosa." Alama10)*Kyo*
5. "Z.Burhani alifaulu sana kukipa kitabu chake anwani mwafaka"Jadili. (Alama 20) *Kyo*
HADITHI FUPI: MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE.
MKIMBIZI: John Habwe.
6. (a)
i Kwa kurejelea hadithi ya mkimbizi eleza madhila yanayowakumba au kukabili wakimbizi
(Alama10)*Kyo*
ii Ni mafunzo yapi yoyote mawili tunayoweza kujifunza kutoka kwa hadithi ya mkimbizi
(Alama 4) *Kyo*
iii Taja na uelezee sifa zozote tatu za Mzee Savalanga. (Alama 6) *Kyo*
AU
UTEUZI WA MOYONI: R ayya Timammy.
(b) "We mwanamke! We! Unataka kunitawala? Nimekuoa au umenioa? Huniamini nikikwambia ni kazi?"
i El e zea muktadha wa dondoo hili (Alama 4) *Kyo*
ii Onyesha jinsi ambavyo taasubi za kiume zimemtawala mzungumzaji katika dondoo hili
(Alama4) *Kyo*
iii Elezea sifa zozote mbili za mzungumzaji ukirejelea dondoo hili (Alama2) *Kyo*
iv "Matatizo wanayoyapitia wanawake ni mengi." Fafanua kauli hii ukirejelea hadithi ya uteuzi wa
moyoni (Alama10) *Kyo*
FASIHI SIMULIZI
7. (a) zingatia kitendawili hiki.
Kitendawili ! Tega
Mzee huyu haachi nyumba yake.
Jawabu ni kobe.
i Vitendawili huwa katika kipera kipi cha fasihi simulizi. (Alama 1) *Kyo*
ii Elezea muundo wa kitendawili ulichopewa. (Alama 3) *Kyo*
iii Vitendawili vilikuwa na umuhimu gani katika jamii? (Alama 6) *Kyo*
(b) Jibu maswali kama ulivyoagizwa .
i Taja vipera viwili vya mazungumzo katika fasihi simulizi (Alama 2) *Kyo*
ii Tofautisha dhana zifuatazo (Alama 2) *Kyo*
• Mighani
• Miviga
iii Taja sifa bainifu za ngano (Alama 4) *Kyo*
(c) Fumbua fumbo hili. (Alama 2) *Kyo*
chura ameanguka katika shimo lenye kina cha mita thelathini. Lakini yeye anaweza kuruka juu mita kumi pekee, je itamlazimu aruke mara ngapi ndipo atoke shimoni?






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers